Welcome to the blog of Mr. Chesco Kilemile who is a renowned singer who came on in the industry singing gospel music. If you like this blog tourism will get to know my work and events relating to the preparation of my work in general ..... thank you for visiting this blog .....

Monday, November 24, 2014

TUCTA yataka waliochota fedha za Escrow kujitathimi

TUCTA YATAKA WALIOCHOTA FEDHA ZA ESCROW WAJITATHIMINI. SHIRIKISHO la Wafanyakazi Nchini(Tucta), limesema haliridhishwi na namna sakata la uchotwaji wa fedha za Escrow linavyoshughulikiwa na kuwatakawahusika wote wanaotajwa kuanza kujitathimini kama wanafaa kuendelea na nyadhifa zao. Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Rais wa Shirikisho hilo, Gracian Mukoba, alisema wamechoshwa na taarifa za wizi wa fedha za umma kila kukicha na kuongeza kuwa hili la Escrow linashughulikiwa taratibu kwa kuwa baadhi ya vigogo au ndugu zao wanahusika nalo. Mukoba alisema kama Tucta wangependa kuona si tu wahusika waishie kujiuzulu bali wafikishwe katika vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kuiba fedha za umma. “Ni jambo la kushangaza kwamba wizi huu unatetewa kwa nguvu zote na baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali wakiwemo baadhi ya Wabunge wanaojali zaidi maslahi yao binafsi. “Wizi huu ni ishara kuwa nchi inaelekea kubaya kwa vile kamwe Watanzania wanyonge walio wengi hawawezi tena kushuhudia fedha na rasilimali zao zikiibiwa na kunufaisha wachache huku wakikabiliana na hali ngumu ya maisha na umasikini uliokithiri,” “Kwa mujibu wa Mukoba mtu aliyekata tamaa ya maisha haogopi kufa na haya ndiyo yaliyotokea katika nchi ya Bukinafaso hivi karibuni na kwingineko ingawa hawatuombei yatokee hapa kwetu,” alisema. Hata hivyo alidai kuwa hii ni sehemu ndogo tu ya wizi unaoendelea nchini na wahusika hawana wasiwasi kwa vile wanajua kama ilivyokuwa EPA na hili pia litapita bila kuwaletea madhara yoyote. Aliongeza kuwa hawa watu ambao sio wenzetu hawana hofu ya kuiba kwa vile hakuna wa kuwauliza kwani kumesharipotiwa wanyamapori wanaibiwa na kusafirishwa nje ya nchi huku vyombo vya ulinzi na usalama vikishuhudia. Pia madini yanachimbwa kila kona ya nchi lakini hayana manufaa kwa taifa kutokana na mikataba mibovu inayolenga kuwanufaisha wachache. “Ieleweke kwamba wizi wa namna hii unaoendelea nchini ndio unaokwamisha jitihada za kupatikana kwa mishahara bora inayokidhi mahitaji ya msingi ya maisha na ndio unaokwamisha ulipaji wa madeni ya muda mrefu ya walimu na watumishi wengine wa umma.

No comments:

Post a Comment